IQNA

Wasomi wa Tunisia watahadharisha juu ya hatari ya Uwahabi

23:23 - August 22, 2012
Habari ID: 2397265
Maulamaa na wasomi wa Tunisia wametahadharisha juu ya uwekezaji wa nchi za Qatar na Saudi Arabia katika kueneza fikra za Kiwahabi nchini Tunisia na wamewataka wananchi kuwa macho mbele ya hatari ya kutumbukia katika vita vya kimadhehebu.
Wizara ya Utamaduni ya Tunisia imetoa taarifa ikitangaza kuwa kufuatia hujuma iliyofanywa na kundi la Masalafi (Mawahabi) dhidi ya washiriki katika Kongamano la al Aqsa katika mji wa Benzert nchini Tunisia na kukaririwa mashambulizi kama hayo dhidi ya makongamano yaliyofanyika kwenye miji mbalimbali ya nchi hiyo, Wizara ya Utamaduni inalaani vikali harakati hiyo hatari. Imeitaja harakarti hiyo kuwa inapingana na uhuru wa kujieleza na inaeneza fikra finyu katika jamii yenye misimamo ya wastani ya Watunisia.
Wizara ya Utamaduni ya Tunisia imezitaka pande zote kukabiliana na hatua hizo za makundi yenye misimamo mikali.
Wakati huo huo Abdul Fattah Moro ambaye ni miongoni mwa viongoziwa ngazi za juu wa chama cha al Nah’dha ametahadharisha juu ya hatua zinazofanywa na wahubiri wa Kisaudia wanaoongoza ratiba na mipango ya kueneza fikra za Kiwahabi nchini Tunisia.
Amesema wahubiri wa Saudia wamekuwa wakitoa mafunzo ya muda kwa vijana wa Kitunisia na kuwapa fedha. Ameongeza kuwa suala hilo ni hatari kubwa kwa sababu linatishia usalama wa nchi na kufungua mlango wa fitina nchini Tunisia.
Kamal al Sakir ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Waarabu na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Tunisia amesisitiza kuwa nchi hiyo inakaribia kutumbukia katika dimbwi la fitina na kwamba fikra za Kiwahabi zimeingia na kuenea nchini humo kwa msaada wa dola za nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na wahubiri wa Kiwahabi.
Amesema fikra za kidini za Saudia ni finyu mno na hazioani na mantiki na akili na kuongeza kuwa, baadhi ya nchi za Ghuba ya Uajemi ikiwemo Saudi Arabia na Qatar, zinawekeza kwa ajili ya kueneza fitina za kimadhehebu na kuitumbukiza Tunisia katika vita vya kidini.
Alkhamisi iliyopita kundi moja la Kiwahabi lilivamia Kongamano la al Aqsa katika mji wa Benzert nchini Tunisia na kujeruhiwa watu 5. 1082979


captcha