IQNA

Maonyesho ya nakala ya kale ya Qur’ani Tukufu huko Kashmir

15:30 - August 25, 2012
Habari ID: 2398413
Nakala ya kale ya Qur’ani Tukufu iliyoandikwa kwa hati za mkono mwaka 1237 Hijria na kutarjumiwa kwa lugha ya Kifarsi inaonyeshwa katika maaonyesho ya jimbo la Kashmir huko India.
Tovuti ya al Hind al Youm imeripoti kuwa, nakala hiyo ya Qur’ani Tukufu iliandikwa na msanii na mwanakaligrafia mashuhuri wa Kashmir Fathullah na inaonyeshwa sasa katika maonyesho ya eneo hilo.
Nakala hiyo ya Qur’ani Tukufu inatambuliwa kuwa ya kale zaidi ya Qur’ani zilizoandikwa kwa hati za mkono katika eneo la Kashmir na kugunduliwa kwake kunaonyesha historia ya miaka mingi huko nyuma ya Waislamu katika eneo hilo la dunia.
Katibu wa Akademiaa ya Sanaa, Utamaduni na Lugha ya majimbo ya Jamu na Kashmir huko India anasema kuwa nakala hiyo ya kale ya Qur’ani ina tarjumi ya Kifarsi.
Khalid Bashir ameongeza kuwa nakala hiyo ya Qur’ani iliandikwa mwaka 1237 Miladia. 1083796
captcha