Shirika rasmi la habari la Palestina limeripoti kuwa katika sherehe hiyo ambayo imehudhuriwa na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas, mahafidhi kadhaa wa Qur’ani wa Palestina walioshiriki katika mashindano ya kimataifa katika nchi za Imarati, Kuwait na Palestina kwenyewe na kushika nafasi za juu wameenziwa na kutunukiwa zawadi.
Walioenziwa katika sherehe hiyo ni Daud Abdullah Abyat aliyeshika nafasi ya kwanza katika mashindano ya hifdhi ya Qur’ani Tukufu ya Kuwait, Ahmad al Adam aliyeshika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya al Aqsa na Ahmad Badii Taha ambaye pia alishina nafasi nzuri katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Imarati.
Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewapongeza mahafidhi na makarii hao kwa kushika nafasi za juu katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani na akasema anawaunga mkono mahafidhi wote wa madrasa na vyuo vikuu vya Palestina.
Mahmoud Abbas pia amewahamasisha mahafidhi hao wa Qur’ani kudumisha mwenendo huo na kuwafunza wengine Qur’ani Tukufu.
Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na viongozi wengine wa ngazi za juu ya serikali ya Palestina. 1084898