Msikiti huo ni miongoni mwa maeneo ya kihistoria ya Libya na kandokando yake kuna makaburi ya maulamaa wa Kiislamu ambayo yanatembelewa na waumini kwa ajili ya kuwasomea dua na al Fatiha.
Hoja kuu iliyotumiwa na Mawahabi hao ni kuwa eneo hilo linatumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kufanya bidaa na hurafa.
Ijumaa iliyopita pia Mawahabi hao wenye misimamo mikali walivamia na kuharibu kaburi na mwanazuoni mwingine wa Kiislamu katika mji wa Ziltan ulioko umbali wa kilomita 160 kutoka Tripoli.
Vitendo hivyo vya kuvunja athari za kale na makaburi ya viongozi wa Kiislamu ni uzushi ulioanzishwa na Saudi Arabia baada ya kushambulia na kuvunja makaburi ya masahaba na Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) katika eneo la Baqii mjini Madina.
1085027