IQNA

Misri yafungua kivuko cha Rafah

14:17 - August 27, 2012
Habari ID: 2400055
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Palestina imetangaza kuwa serikali ya Misri imesema itafungua kikamilifu kivuko cha mpakani cha Rafah na kwamba kivuko hicho kitakuwa wazi katika siku zote za wiki isipokuwa Ijumaa.
Uamuzi huo wa Misri utaukasirisha mno utawala ghasibu wa Israel ambao unatelekeza vikwao na mzingiro wa pande zote dhidi ya raia zaidi ya milioni moja wa Ukanda wa Gaza kwa miaka kadhaa sasa.
Serikali mpya ya Misri ilifungua tena kivuko cha Rafah ambacho kilifungwa kabisa na serikali ya dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak ambaye alishirikiana na utawala ghasibu wa Israel kuwatesa na kuwanyanyasa raia wa Ukanda wa Gaza. Hata hivyo kivuko hicho kilifungwa tena mapema mwezi huu baada ya shambulizi lililowalenga askari usalama wa Misri katika jangwa na Sinai na kuua askari 16.
Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema shambulizi hilo lilipangwa na Israel ili kuilazimisha Misri ifunge tena kivuko hicho muhimu kwa maisha ya watu wa Gaza. 1084923
captcha