Maonyesho hayo yanafanyika kwa ushirikiano wa Kituo cha Masuala ya Kidini cha China na Jumuiya ya Masuala ya Kidini ya Uturuki kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa kiutamaduni wa nchi hizo mbili.
Maonyesho hayo yatajumuisha nakala za kale za Qur'ani zilizoandikwa kwa hati za mkono, matunda ya kiutamaduni na Kiislamu ya Waislamu wa China na maonyesho ya kaligrafia.
Sehemu moja ya maonyesho hayo itahusu kazi za wasanii wa Kiislamu wa China na athari za kihistoria na kiutamaduni za miaka 300 iliyopita. 1086853