Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa askari sita wa Marekani ambao wanadai hawakuchoma nakala hizo za Qur’ani Tukufu kwa makusudi, jana walitambuliwa na mahakama ya nchi hiyo kuwa hawana hatia na kwamba watapewa adhabu ndogo ya kiidara. Hata hivyo shirika hilo la habari la Marekani halikutoa habari zaidi kuhusu adhabu eti ya “kiidara”.
Kwa kawaida adhabu ya kiidara huwa na maana ya kushushwa cheo, kukatwa mshahara, kutoa ahadi ya kutokariri kosa au kufukuzwa jeshini.
Kitendo cha askari hao sita wa Marekani cha kuchoma moto nakala za kitabu kitakatifu cha Qur’ani kulizusha maandamano makubwa nchini Afghanistan na ameneo mengine ya dunia na watu kadhaa wakiwemo askari wa Marekani waliuawa katika machafuko hayo.
Hukumu hiyo dhaifu iliyotolewa na mahakama ya Marekani dhidi ya wahalifu hao pia huenda ikazusha upinzani na maandamano makubwa nchini Afghanistan na kwengineko.
Msemaji wa Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema ofisi ya kiongozi huyo inachunguza uamuzi uliochukuliwa kuhusu askari hao wa Marekani na itatoa mtazamo wake kuhusu suala hilo hivi karibuni. 1087031