Kanali ya Kiarabu ya Haki za Binadamu imelaani kitendo hicho cha askari cha kuwafyatulia risasi watu waliokuwa wakifanya mandamano ya amani na kutishia kuwaua.
Kanali hiyo imelaani ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukandamizaji wa haki za kujieleza nchini Saudia sambamba na kimya cha jamii za Kiarabu na kimataifa na imezitaka nchi mbalimbali kuishinikiza Saudi Arabia na kuitaka iruhusu maandamano ya amani na wapinzani wake.
Vilevile imeitaka Saudi Arabia kuwaachia huru watu waliotiwa mbaroni katika maandamano hayo ya amani na kuheshimu haki za binadamu.
Familia za watu wanaoshikiliwa katika mahabusu za utawala wa Saudi Arabia zilifanya maandamano Jumapili iliyopita mbele ya jela ya al Hair mjini Riyadh ambayo yalikandamizwa kwa mashambulizi ya askari usalama. Waandamanaji hao waliitaka serikali ya Riyadh iwaruhusu kukutana na jamaa zao wanaoshikiliwa bila ya kufikishwa mahakamani. 1087407