IQNA

18:20 - August 31, 2012
Habari ID: 2402148
Rais Ahmadinejad:

Utawala wa Kizayuni na nchi za kibeberu za Magharibi ni tishio kwa mataifa mbalimbali

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, utawala wa Kizayuni na mataifa ya kibeberu ya Magharibi ni tishio kwa usalama wa nchi zote za eneo la Mashariki ya Kati.

Rais Ahmadinejad aliyasema hayo hapo jana alipofanya mazungumzo na Rais wa Misri Muhammad Mursi hapa mjini Tehran na kusisitiza kuwa, utawala katili wa Kizayuni na madola ya Magharibi hususan Marekani, ni tishio kwa usalama wa mataifa ya Mashariki ya Kati na ulimwengu mzima kwa ujumla.
Amesema, kamwe mabeberu hawajawahi kuyatakia kheri, maendeleo na uwezo wa kujitegemea mataifa huru yanayopigania uadilifu duniani na kwamba, maadui wanaamiliana na mataifa mengine duniani kwa kuangalia tu manufaa yao ya muda mrefu katika mataifa hayo.
Vilevile ameashiria tamaduni za pamoja kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Misri na kusema kuwa, Misri inayo nafasi kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, ikiwa mataifa ya Misri na Iran yatashirikiana basi suala hilo litakuwa na manufaa makubwa kwa nchi hizi.
Kwa upande wake Rais Muhammad Mursi wa Misri, ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuwa mwenyekiti wa mkutano wa 16 wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) na kusema, hisia za urafiki na udugu kati ya watu wa Iran na Misri zilikuwepo tangu zamani sana. 1088405
captcha