Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha Lebanon ameeleza kuwa, ufumbuzi wa kisiasa na kufanyika mazungumzo kati ya serikali ya Syria na wapinzani ndiyo njia ya busara ya kutatua mgogoro wa nchi hiyo.
Sayyid Nasrullah pia amesema, mgogoro wa Syria hauwezi kupatiwa ufumbuzi iwapo hakutakuweko na usitishaji mapigano utakaofuatiwa na mazungumzo kati ya pande zote husika huko Syria.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameisifu serikali ya Damascus kwa hatua yake ya kuyaalika makundi ya upinzani kwenye meza ya mazungumzo na kuwakosoa waasi wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi kwa kupinga pendekezo hilo la serikali ya Syria.
Sayyid Nasrullah pia amemuunga mkono Rais Bashar Assad na kusema kuwa nchi za Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu zinajaribu kila linalowezekana kuiangusha serikali ya Syria kutokana na msimamo wake ya kuupinga utawala wa Kizayuni wa Israel. 1091005