Mwakilishi wa Iran katika sehemu ya kiraa ya mashindano hayo ya kimataifa ameiambia IQNA kwamba sherehe hiyo ilipangwa kuanza mapema leo na kuendelea hadi jioni.
Hassan Danesh amesema kuwa makarii kutoka nchi 20 wamechuana katika mashindano hayo ya kimataifa na kwamba mchuano mkali zaidi ulikuwa katika ya makarii kutoka Misri, Libya, Algeria, Yemen na Morocco.
Mwakilishi wa Iran katika upande wa kiraa ya Qur'ani kwenye mashindano hayo amesema, yamefanyika kwa kiwango cha juu na ameeleza matarajio ya kupata nafasi ya kwanza kama ilivyokuwa katika mashindano ya mwaka jana.
Akilinganisha mashindano hayo ya Tunisia na yale ya kimataifa yanayofanyika nchini Iran, Hassan Danesh amesema mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran hufanyika kwa utaratibu wa aina yake na hayawezi kulinganishwa na mashindano kama hayo yanayofanyika katika nchi nyingine hususan kwa kuzingatia kwamba huwashirikisha makarii na mahafidhi wengi kutoka nchi mbalimbali duniani. 1091323