Tovuti ya Palestine Info imenukuu Omar Mahfudhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kiislamu cha Ottawa akisema kuwa: "Tunapaswa kukubali kwamba tunaishi katika jamii ya Kikristo na hatuna uwezo wa kusikiliza hata sauti ya adhana katika nyakati za swala."
Ameongeza kuwa hadi sasa sauti ya adhana haijawahi kusikika katika misikiti ya miji mbalimbali ya Canada.
Waislamu wanaunda asilimia 1.9 ya jamii ya watu milioni 32.8 ya Canada na Uislamu unahesabiwa kuwa dini kubwa ya pili nchini humo baada ya Ukristo. Mjini Ottawa Waislamu wanaunda asilimia 3.9.
Kati ya misikiti 8 ya Ottawa ni msikiti mmoja tu wenye mnara ambao pia hauruhusiwi kutumiwa kwa ajili ya kutoa adhana.
Sauti ya adhana misikitini imepigwa marufuku nchini Canada na misikiti na vituo vya Kiislamu vinaweza kutumia adhana ndani ya misikiti tu bila ya kusikika nje.
Waislamu wa Canada hutambua nyakati za swala kupitia mtandao wa intaneti.
Katika baadhi ya nchi za Ulaya pia ujenzi wa minara kwa ajili ya adhana umepigwa marufu. 1091386