IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Wanachuo Waislamu yaanza Tabriz

17:20 - September 12, 2012
Habari ID: 2410260
Duru ya nne ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanafunzi Waislamu wa Vyuo Vikuu yameanza leo katika mji wa Tabriz uliokpo magharibi mwa Iran yakiwashirikisha wanavyuo waliohifadhi Qur'ani nzima kutoka nchi mbalimbali.
Mashindano hayo yamefunguliwa kwa kiraa ya karii mashuhuri wa Misri Ustadh Shadhili katika ukumbi wa swala wa Imam Khomeini.
Washiriki katika mashindano hayo wanachuana katika hifdhi ya Qur'ani nzima na kiraa katika vipindi viwili vya asubuhi na alasiri.
Duru hii ya mashindano ya Qur'ani ya wanachuo Waislamu inawachuanisha wanafunzi 74 wa vyuo vikuu kutoka nchi 52 na itaendelea kwa kipindi cha siku tatu kabla ya kufungwa Ijumaa ijayo katika sherehe rasmi za kugawa zawadi kwa washindi.
Nchi nyingi zaidi zimeshiriki katika duru hii ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu. Nchi 40 pekee zilishiriki katika duru ya tatu ya mashindano hayo. 1096940

captcha