Fainali ya mashindano hayo ilifunguliwa kwa kiraa ya Ustadh Abdul Fattah al Taruti ambaye alikuwa miongoni mwa majaji wa mashindnao hayo kutoka Misri.
Sehemu ya hifdhi ya Qur’ani nzima ilishirikisha washindani saba na kiraa ilikuwa na washindani 6.
Katika mashindano ya hifdhi ya Qur’ani nzima Abu Dharr Karami wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameshika nafasi ya kwanza baada ya mchuano mkali uliokuwa na mahafidhi kutoka nchi za Mauritania, Misri, Indonesia, Tajikistan, Uganda na Qatar.
Katika upande wa kiraa ya Qur’ani, Majiid Faqihi wa Jamhuri ya Kiislamu ameshika nafasi ya kwanza na kuwaacha nyuma makarii kutoka Lebanon, Kuwait, Ujerumani, Afghanistan na Bahrain.
Sherehe za kuhitimisha duru ya 4 ya mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya wanafunzi Waislamu wa vyuo vikuu zilianza mapema jana. Mashindano hayo yamewashirikisha wawakilishi wa nchi 52. 1098364