Gazeti la al Dustur limeripoti kuw,a kiwanda hicho kimekuwa kikichapisha, kusambaza na kuuza nakala za Qur’ani Tukufu bila ya ruhusa ya Jumuiya ya Utafiti wa Kiislamu ya al Azhar na wakati wa kutiwa nguvuni mmiliki wake Muhammad Ahmad Ridhwan kumekamatwa nakala 2590 kiwandani hapo ambazo zimechapishwa bila ya kibali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri Usama al Saghir ameliamuru jeshi la polisi kumtia mbaroni mmiliki wa kiwanda hicho na kumkabidhi kwa vhombo vya sheria kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa zaidi ya asilimia 60 ya nakala za Qur’ani Tukufu kote duniani zinachapishwa nchini Misri na katika siku za hivi karibuni baadhi ya viwanda vya uchapishaji nchini humo vimetuhumiwa kuwa vimechapisha nakala za Qur’ani zenye makosa makubwa ya kichapa ambazo baadhi yazo zimetumwa katika nchi za nje. 1107390