Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la nchi hiyo SUNA, tamasha hilo litaandaliwa na Wizara ya Mwongozo wa Kiislamu na Wakfu ya Sudan.
Lengo la tamasha hilo limetajwa kuwa ni kuwashajiisha raia wa Sudan na hasa tabaka la vijana wazingatie Qur'ani Tukufu kwa ushirikiano wa wanazuoni, watafiti na wanafikra wa Kiislamu wa nchi hiyo.
Tamasha hilo hufanyika kila mwaka katika mojawapo ya majimbo ya nchi hiyo ambapo rais wa nchi hushiriki katika sherehe za ufungaji wake. Shughuli mbalimbali za mahubiri ya kidini pia hufanyika katika tamasha hilo. 1108771