IQNA

London mwenyeji wa kongamano la kimataifa la Ukurubishaji wa Madhehebu ya Kiislamu

14:23 - September 29, 2012
Habari ID: 2421904
Kongamano la nane la Ukurubishaji wa Madhehebuya Kiislamu ambalo limeandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Uingereza limepangwa kuanza leo Jumamosi mjini London.
Kongamano hilo linafanyika chini ya anwani ya 'Nafasi ya Ustaarabu wa Ukurubishaji katika Kuhudumia Amani ya Kijamii.'
Abdul Aziz bin Othman at-Tuwejiri, Katibu Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) amepangiwa kutoa hutuba ya ufunguzi wa kongamano hilo ambapo atazungumzia mpango wa kukabiliana na fikra za kupindukia mipaka na ukufurishaji wa Waislamu.
Thamani za ukurubishaji wa madhehebu ya Kiislamu katika kukabiliana na hujuma ya kiutamaduni dhidi ya umma wa Kiislamu, changamoto zinazowakabili Waislamu waliowachache, ushirikiano wa Waislamu kwa ajili ya kuimarisha amani ya kijamii, nafasi ya wanawake katika kulea familia na jamii bora na nguzo za amani ya kijamii pamoja na athari zake katika kustawisha jamii ya mwanadamu ni masuala muhimu yatakayojadiliwa katika kongamano hilo. 1109096
captcha