IQNA

Russia yapiga marufuku filamu inayomtusi Mtume SAW

14:53 - September 29, 2012
Habari ID: 2422173
Mahakama ya Russia imetangaza kuwa, ni marufuku nchini humo kuonyeshwa filamu iliyotengenezwa Marekani ambayo inamtusi na kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Mahakama ya Russia imeeleza kwamba, filamu hiyo haipaswi kuonyeshwa nchini humo, kwani inamvunjia heshima Mtume SAW, na inapingwa na Waislamu kote ulimwenguni.

Wakati huohuo, Waislamu nchini Afrika Kusini walifanya maandamano makubwa jana wakilaani vikali utengenezwaji wa filamu hiyo na kusisitiza kwamba kamwe hawatakubali kuona matukufu ya Kiislamu yakidhalilishwa na kuvunjiwa heshima.

Waislamu wa mjini Johannesburg walikusanyika mbele ya Ubalozi mdogo wa Marekani mjini humo, na kupiga nara dhidi ya Marekani. Aidha Waislamu hao wameitaka serikali ya Marekani kuwatia mbaroni wale wote waliohusika katika kutengeneza filamu hiyo inayotusi matukufu ya Kiislamu sanjari na kupigwa marufuku nchini humo.
1109075
captcha