Usama al Mazini amesema kuwa, wataalamu wa Kipalestina wamefanikiwa kutengeneza programu ya kwanza ya tarjumi ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya ishara itakayotumiwa na viziwi. Ameongeza kuwa kazi hiyo itazinduliwa hivi karibuni.
Programu hiyo ya tarjumi ya Qur'ani kwa lugha ya ishara imetengenezwa kwa usimamizi wa Wizara ya Elimu ya Juu na kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mustakbali wa Viziwi na Taasisi ya Nyumba ya Qur'ani.
Programu hiyo inajumuisha CD ya juzuu 30 za Qur'ani Tukufu. 1110290