IQNA

16:43 - October 02, 2012
Habari ID: 2424664
Salman Rushdie:

Ninahisi hatari kutokana na kuchapishwa tena fatuwa ya Imam Khomeini

Mwandishi wa kitabu cha "Aya za Shetani" murtadi Salman Rushie amesema kuwa, kuchapishwa tena fatuwa ya Imam Khomeini aliyemhukumu kifo mwandishi huyo, katika mitandao ya kijamii kwenye intaneti kunamtia woga na wahaka mkubwa.

Kituo cha FranceTv kimeripoti kuwa Rushie alisema jana katika kikao cha waandishi habari kilichofanyika Berlin huko Ujerumani kwamba, fatuwa ya kifo iliyotolewa na hayati Imam Ruhullah Khomeini mwaka 1988 imekuwa na taathira kubwa katika medani ya kimataifa na kuongeza kuwa, fatuwa hiyo ilitolewa katika kipindi ambacho mawasiliano baina ya watu yalitegemea simu na fax pekee lakini hii leo anahisi hatari zaidi kwa sababu fatuwa hiyo inasambaa kwa kasi sana katika mitandao ya intaneti na mitandao ya kijamii kama Facebook na Twiter.
Mwandishi huyo aliyevunjia heshima matukufu ya Kiislamu ameendelea kuwa, kasi ya upashaji habari imekuwa kubwa zaidi na tukio lolote linalotokea kwenye kona ya dunia linaenea kwa kasi, suala ambalo amesema linazidisha hatari kwa watu kama yeye.
Salman Rushdie amekuwa akiishi mafichoni tangu mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini alipomhukumu kifo baada ya kuandika kitabu cha Aya za Shetan (Satanic Verses) kinachomtusi na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na matukufu mengine ya Kiislamu. 1111801

captcha