IQNA

Waislamu na Wakristo wa Lebanon walaani filamu iliyo dhidi ya Uislamu

19:48 - October 02, 2012
Habari ID: 2424699
Waislamu na Wakristo wa mji wa Hasibiyya nchini Lebanon jana Jumatatu walifanya kikao cha pamoja cha kulaani filamu ya matusi inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) iliyotengenezwa huko Marekani kwa ushirikiano wa Wazayuni wa Israel.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi wa kisiasa na kidini wa Lebanon kilifanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Hasibiyya. Wamesisitiza kwamba Wazayuni ndio waliokuwa na mchango mkubwa katika utengenezaji wa filamu hiyo inayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu. Wamesema Wamarekani na Wazayuni daima wamekuwa wakitekeleza njama za kueneza fikra zilizo dhidi ya Uislamu na Ukristo ili kupenyeza fikra za uzayuni mamboleo miongoni mwa walimwengu, na hasa mataifa ya Mashariki ya Kati na Asia.
Taarifa ya mwisho ya kikao hicho imelaani vikali njama hizo na kusema kuwa, kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu na Kikristo ni aina moja ya ugaidi wa kifikra unaodhaminiwa na Marekani na utawala haramu wa Israel.
Pia imeshukuru hatua ya makanisa ya Lebanon ya kulaani vikali filamu hiyo na kukemea vikali hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuiomba msamaha Marekani kutokana na kushambuliwa balozi zake katika nchi hizo, ikisema kuwa hiyo ni dharau ya moja kwa moja kwa Waislamu.
Taarifa hiyo imesema hali hiyo inatokana na ukweli kuwa Marekani ambayo inaeneza siasa za chuki dhidi ya Uislamu ndiyo inayopasa kuwaomba msamaha Waislamu kwa sababu ndiyo iliyoanzisha uchokozi na dharau dhidi yao kwa kuruhusu kutengenezwa filamu hiyo. 1111942
captcha