IQNA

16:56 - November 06, 2012
Habari ID: 2443935
Jumuiya za Kiislamu:

Waislamu kote duniani wafanye maandamano ya kuwatetea wenzao wa Myanmar

Jumuiya 11 za Kiislamu katika nchi za Ulaya na Asia zimetoa wito wa kufanyika maandamano ya kuonesha mshikamano wa kimataifa na Waislamu wa Myanmar wanaoendelea kuuawa ovyo.

Wito ulitolewa na jumuiya hizo umewataka Waislamu kote duniani kufanya maandamano makubwa Alkhamisi ijayo na kuwatetea Waislamu wenzao wanaoendelea kuuawa na kukandamizwa na Mabudha wenye misimamo mikali nchini Myanmar.
Taarifa ya jumuiya hizo imewataka Waislamu kote duniani kufanya maandamano mbele ya balozi za Myanmar na kuonesha mshikamano wao na wenzao wanaouawa kwa umati nchini Myanmar.
Taarifa ya jumuiya hizo imewataka waandamanaji hao waunge mkono suala la kutumwa askari wa kimataifa wa kulinda amani nchini Myanmar, kuruhusiwa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya maeneo ya Waislamu, kutumwa kamati ya kutafuta ukweli ya Umoja wa Mataifa nchini humo na kukomeshwa ukatili na mauaji yanayofanywa na Mabudha dhidi ya Waislamu.
Mauaji na ukatili unaofanywa na Mabudha waliowengi nchini Myanmar dhidi ya Waislamu umeitia wasiwasi mkubwa jamii ya kimataifa.
Waziri Mkuu wa Australia Julia Gillard amewatahadharisha viongozi wa serikali ya Myanmar na kuwataka waboreshe hali ya haki za binadamu nchini humo. Vilevile Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ulaya José Manuel Barroso ametembelea Myanmar na kuitaka serikali ya Nay Pyi Taw ikomeshe ukatili dhidi ya Waislamu. 1132269

captcha