IQNA

UN yaitaka Myanmar kuwatambua Waislamu wa Rohingya kuwa ni raia

19:34 - November 10, 2012
Habari ID: 2445759
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Myanmar kuwapa haki za kiraia Waislamu nchini humo.
Navi Pillay ambaye alikuwa akihutubia katika Mkutano wa Kimataifa wa Demokrasia huko Bali, Indonesia amesema serikali ya Myanmar inapaswa kuchukua hatua za kuwapa haki za kiraia Waislamu wa kabila la Rohingya na kuamiliana nao kwa uadilifu.
Vilevile ameitaka Myanmar kubadili sheria za sasa za nchi hiyo na kuwaruhusu Waislamu kuwa na haki ya uraia. Pillay amesema Umoja wa Mataifa una wasiwasi mkubwa kuhusu ukandamizaji na juhudi zinazofanywa nchini Myanmar kwa ajili ya kuangamiza jamii ya Waislamu wa Rohingya.
Takwa hilo la Umoja wa Mataifa la kupewa uraia Waislamu wa Myanmar limetolewa siku moja tu baada ya wanaharakati wa haki za binadamu wa kimataifa kutoa wito wa kupelekwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Myanmar kwa shabaha ya kukomesha ukandamizaji na mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu wa magharibi mwa nchi hiyo. 1134445


captcha