Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast pia amesema kuwa, mashambulizi ya kijeshi ya utawala haramu wa Israel huko Gaza yanayopelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya wananchi wa Palestina kwa mara nyingine yanathibitisha hatua za kikatili za utawala huo.
Mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza yaliyosababisha kuuawa shahidi Wapalestina kadhaa yamelaaniwa na kukabiliwa na radiamali kali ya jamii ya kimataifa.
Rais Muhammad Morsi wa Misri kupitia msemaji wake amelaani jinai hizo na kulitaka Baraza la Usalama kuitisha kikao cha dharura kujadili mashambulizi hiyo. Pia kufutia mashambulizi hayo Misri imemwita nyumbani balozi wake huko Israel.
1137767