IQNA

Vitendo vya matakfiri vinamtukanisha Mtume SAW

16:09 - January 10, 2015
Habari ID: 2692014
Katibu Mkuu wa chama cha Hizbullah cha nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah, amesema kuwa vitendo vinavyofanywa na makundi ya kigaidi na kitakfiri, ninamtukanisha Mtume Muhammad SAW, Qur'ani na umma wa Kiislamu.

Sayyid Hassan Nasrullah aliyasema hayo jioni ya jana katika sherehe za kukumbuka mazazi ya Mtume wa Uislamu, Muhammad al Mustafa SAW na mjukuu wa mtukufu huyo, Imam Jaafar Swadiq AS zilizofanyika sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Umoja huko Bairut, mji mkuu wa Lebanon na kuongeza kuwa, watu ambao wanakata vichwa vya watu wengine, hawawezi kamwe kudai kuwa wanamtetea Mtume Muhammad SAW. Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon amesema kuwa, vitendo vya kuitukanisha dini tukufu ya Kiislamu vinavyofanywa na makundi ya kitakfiri, havijawahi kushuhudiwa mfano wake katika historia ya Kiislamu. Amesema kuwa, kuna udharura wa kuutetea Uislamu na kuusafisha na dhana potofu za makundi hayo ya kigaidi, kama vile alivyofanya Imam Hussein AS, mjukuu wa Bwana Mtume SAW katika jangwa la Karabala, kwani huo ni wadhifa wa kila Muislamu. Aidha Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, wanamapambano wa Hizbullah kwa kushirikiana na jeshi la Lebanon wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kulinda mipaka ya nchi hiyio kutokana na makundi hayo yanayowakufurisha Waislamu wengine na wanalihesabu kuwa ndilo jukumu lao na jukumu la kila mfuasi sahihi wa Mtume Muhammad SAW.../mh

2688566

captcha