IQNA

Sayyid Hassan Nasrullah

Saudia imeshindwa kufikia malengo yake Yemen

16:59 - May 06, 2015
Habari ID: 3262998
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa Saudi Arabia haijafikia malengo yake katika uvamizi wa kijeshi ilioanzisha huko Yemen.

Sayyid Hassan Nasrullah, ameashiria mashambulizi makubwa ya kikatili  na madai ya Saudi Arabia kuhusu kufikia malengo yake huko Yemen na kueleza kuwa, ni wazi kuwa nchi hiyo imegonga mwamba  katika mashambulizi yake nchini Yemen. Amesema Saudi Arabia haijafikia hata lengo lake moja tangu ianzishe mashambulizi yake huko Yemen. Hii ni kwa sababu Abdu Rabbuh Mansur Hadi, Rais wa Yemen aliyejiuzulu  alikimbia huko San'aa na hajarudi tena huku jeshi na vikosi vya wananchi vikizidi kusonga mbele kusini mwa nchi.

Katibu Mkuu wa Hibzullah ya Lebanon amesema kuwa Saudi Arabia na Marekani zimeanzisha mashambulizi ya kijeshi huko Yemen lengo kuu likiwa ni kuidhibiti nchi hiyo na kwamba nchi vamizi zinadai kwamba zinawaunga mkono wananchi wa Yemen, katika hali ambayo ni nyumba za raia ndizo zinazolengwa kwa mashambulizi hayo ya kikatili.../mh

3259544

captcha