Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jumamosi tarehe 30 Mei Ubalozi wa Saudi Arabia huko Senegal uliandaa kongamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Dakar, ambapo wanazuoni na wasomi wa Kiislamu walialikwa katika kongamano lililokuwa na anuani ya ‘Uislamu Unakabiliana na Ugaidi’.
Katika kongamano hilo, mabalozi wa nchi za Waislamu kama vile Misri, Oman, Palestina, Qatar, Morocco n.k walialikwa isipokuwa balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Mbali na wasomi wa Kiwahabbi ambao wanaunga mkono sera za Saudia, pia walialikwa wasomi ambao kidhahiri wana misimamo ya wastani kama vile Profesa Anjai Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Chuo Kikuu cha Dakar na vile vile Shariff Ambalo Mkuu wa Taasisi ya Kishia ya Aal Yaseen. Katika hotuba mbele ya balozi wa Saudi Arabia, Profesa Anjai alikosoa vikali sera za kindumakuwli za Saudi Arabia na kusema utawala wa Aal Saudi ni muungaji mkono mkuu wa ugaidi katika nchi za Kiislamu. Aidha aliulaumu vikali ufalme wa Saudia kwa kuendeleza jinai za kivita nchini Yemen.
Akizungumza katika kongamano hilo, balozi wa Palestina alisisitiza umuhimu wa kutosahauliwa kadhia ya ukombozi wa Palestina.
Hadi sasa Mawahabi hawajafanikiwa kueneza fikra zao nchini Senegal kutokana na kuwa aghalabu ya Waislamu wa nchi hiyo wanafuata tariqa za Kisufi na hivyo hawakubali upotofu wa Uwahabi.../