IQNA

Wanamichezo Waislamu

Mchezaji soka wa Senegal Sadio Mane ashiriki Hija ndogo ya Umrah na wenzake wa Al Nassr

23:13 - August 05, 2023
Habari ID: 3477386
TEHRAN (IQNA)- Mchezaji soka wa timu ya Senegal ambaye amesajiliwa na timu ya Soka ya Al Nassr ya Saudia hivi karibuni, Sadio Mane, ameshiriki katika ibada ya Hija ndogo ya Umrah huko Makka baada ya timu yake kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Zamalek kwenye Kombe la Klabu Bingwa ya Kiarabu 2023.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye alijiunga na Al Nassr kutoka timu ya Bayern Munich katika ligi ya Ujerumani , aliandamana na Waislamu wenzake katika safari hii ya kidini.

Mane, ambaye alisajiliwa na Al Nassr wakati wa usajili wa majira ya kiangazi, aliungana na Seko Fofana na wachezaji wengine katika ibada ya Umrah baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Zamalek. Fofana, ambaye hapo awali aliichezea Lens ya Ligue 1 ya Ufaransa, hivi majuzi alihamia klabu hiyo ya Saudi Arabia. Video ya wachezaji wakiwa katika  Umra baada ya mchezo imesambaa ikionyesha kujitolea kwao kwa imani yao.

Kulingana na ripoti ya Sportstiger.com, Mane na wachezaji wenzake walitumia muda wao wakiwa Makka kutafuta baraka za kiroho na kutoa shukrani zao kwa uchezaji wao katika mechi dhidi ya Zamalek.

Katika mechi dhidi ya Zamalek, Cristiano Ronaldo wa Al Nassr alifunga bao la kusawazisha dakika za lala salama, na kutinga robo fainali ya Klabu Bingwa ya Kiarabu. Ingawa Mane hakuweza kupata bao katika mchezo wake wa kwanza, alienda kwenye Instagram kumshukuru mwenzake mwenye umri wa miaka 38 kwa bao lake muhimu. Mane aliandika, “Une nouvelle page s’ouvre (ukurasa mpya unafunguliwa)!!! Hongera @cristiano!!! Nenda kwa raundi inayofuata. Asante mashabiki wa @alnassr sapoti ilikuwa ya kushangaza."

4160396

Kishikizo: sadio mane senegal umra
captcha