IQNA

ISIS (Daesh) wabomoa msikiti mwingine Iraq

7:21 - August 30, 2015
Habari ID: 3353853
Kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS(Daesh) nchini Iraq, limebomoa msikiti mmoja kusini mwa mkoa wa Nainawa, sanjari na kuondoa nakshi za kihistoria katika makanisa mawili katikati ya mji wa Mosul.

Kwa mujibu wa kanali ya Sumaria News, kundi la Daesh limefanya uharibifu huo Jumamosi ya jana baada ya kuulipua kwa bomu Msikiti wa Abubakar katika viunga vya eneo la al-Shura, kusini mwa mkoa wa Nainawa. Matakfiri hao wasioelewa mafundisho ya dini ya Kiislamu, mbali na kukiri kutekeleza jinai hiyo, wamesema kuwa wameubomoa msikiti huo kutokana na kile walichokitaja kuwa ni kuwepo kaburu ndani yake. Wanachama wa kundi hilo maarufu kwa kutenda jinai pia wameondoa maandishi ya kihistoria katika makanisa mawili ya Bikira Maria na al-Kaldan, katikati mwa mji wa Mosul mkoani Nainawa nchini Iraq. Kabla ya hapo wanachama wa Daesh walifanya mauaji dhidi ya wapiganaji 20 wa kundi hilo mjini Mosul, kwa makosa tofauti ukiwemo usaliti. Si vibaya kukumbusha kuwa, mji wa Mosul umekuwa ukidhibitiwa na wanachama wa kundi hilo la kitakfiri tangu tarehe 10 Juni mwaka 2014, suala ambalo limepelekea mji huo kukumbwa na hali mbaya ya kibinadamu kutokana na wanachama wa kundi hilo kutekeleza sheria kali za kufurutu ada katika mji huo.

3353375

captcha