Mmoja wa waliokamatwa ni mwanamke na mwingine kinara mwandamizi wa kundi hilo la kigaidi, wizara ilisema Alhamisi, Shafaq News iliripoti.
Walikamatwa na polisi wa Jimbo la Nineveh baada ya shughuli za kukusanya taarifa za kiusalama zilizopelekea kuwatambua magaidi hao.
Inakuja wakati msimu wa Arbaeen unakaribia na huku mamlaka ya Iraq ikizidisha juhudi za kuhakikisha usalama wa wafanyaziara.
Magaidi wa Daesh waliwahi kuteka maeneo ya kaskazini na magharibi mwa Iraq katika majira ya joto ya 2014, baada ya kuteka maeneo ya kaskazini mwa Syria.
Baadaye, mseto wa mashambulizi makali ya jeshi la Iraq na vikosi vya kujitolea vilivyoharakisha kuchukua silaha baada ya Ayatullah Sistani kutoa fatwa ya kutaka mapambano dhidi ya magaidi hao na hatimaye walitimuliwa kutoka eneo hilo mwaka 2017.
Hata hivyo kundi hilo la kigaidi bado linaendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo ya mashambani.
Maadhimisho ya Arbaeen hufanyika siku ya 40 baada ya Ashura, ukumbusho adhimu wa kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) ambaye aliuawa shahdii na jeshi la Yazid katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.
Kila mwaka mamilioni ya Mashia na pia idadi ya wasiokuwa Mashia humiminika Karbala, mji ulipo Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS) kufanya ibada za maombolezo. Wafanya ziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri mamia ya kilomita kwa miguu hadi mji mtakatifu wa Karbala.
Arbaeen ya mwaka huu inatarajiwa kuanguka mnamo Agosti 25, kulingana na kuonekana kwa mwezi.
3489432