IQNA

Kufa maji mtoto wa Syria ni aibu kwa jamii ya mwanadamu

18:58 - September 05, 2015
Habari ID: 3358323
Sheikh Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar nchini Misri amesema kufa maji mtoto mkimbizi wa miaka mitatu kutoka Syria katika ufukwe wa Bahari nchini Uturuki ni aibu kwa jamii ya mwanadamu.

Sheikh Ahmed el-Tayeb amesema tukio hilo limedhihirisha namna madola makubwa duniani  yanavyowapuuza mamilioni ya watu wanaopata masiabu kutokana na vita, njaa na maafa mengine.
Amebainisha masikitiko yake kuwa, serikali ambazo zinadai kutetea haki za binadamu zinashuhudia maafa ya wakimbizi pasina kujali.
Sheikh el Tayeb ameashiria hali mbaya ya wakimbizi nchini Syria na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kutekeleza majukumu yake kuhusu maafa katika nchi hiyo.
Picha ya maiti ya mtoto mchanga, Aylan Kurdi, aliyekuwa na umri wa miaka mitatu akiwa amelala kwenye mchanga kwenye pwani ya Aegean kusini magharibi mwa Uturuki imewahuzunisha sana walimwengu baada ya kuchapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii na baadaye magaztini na koneshwa kwenye runinga.


Wakati huo huo baba  yake Aylan Kurdi anaripotiwa kukataa hatua ya Canada ya kumpa makao.
Tima Kurd, ambaye ni dadake Abdullah al Kurdi alisema, alimuambia kuwa anataka kusalia nchini Syria yaliko makaburi ya mkewe na wanawe wawili wa kiume ambao pia walikufa maji nje ya pwani ya Uturuki siku ya jumatano.
Picha ya maiti ya mtoto Aylan Kurdi kutoka Kobani Syria aliyekufa maji akijaribu kuvuuka bahari kuingia Ulaya ingali inaendelea kuutikisa ulimwengu. Eneo la Kobani linakabiliwa na hujuma kali ya magiadi wa ISIS au Daesh wanaopata himaya ya Marekani, Utawala haramu wa Israel na waitifaki wao katika eneo hasa Qatar, Saudi Arabia na Uturuki.
Picha hii inaakisi pia ubaya wa vita vya magaidi wanaopata himaya ya kigeni dhidi ya watu wa Syria. Ni taswira inayochafua nafsi. Ni picha inayomchoma mtu ndani kabisa ya hisia zake kwa mshindo.
Kwingineko Rais Vladmir Putin wa Russia amesema, mgogoro wa wahajiri unaolikabili bara Ulaya kwa sasa umetokana na sera mbovu za kigeni za nchi za bara hilo hususan zile ambazo ni wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU). Kiongozi huyo amesisitiza kuwa, uingiliaji wa Wamagharibi katika mambo ya ndani nchi za Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika ni moja ya sababu za kuibuka mgogoro wa wahajiri katika nchi za EU.../mh

3358055

captcha