IQNA

ISESCO yalaani kushambuliwa Mashia Saudia

18:56 - October 18, 2015
Habari ID: 3388672
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (ISESCO) limelaani vikali hujuma ya kigaidi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa katika majlisi ya maombolezo ya siku 10 za Muharram nchini Saudi Arabia.

Katika taarifa, ISESCO imesema imesikitishwa na hujuma ya kigaidi siku ya Ijumaa dhidi ya ukumbi wa kidini ujulikanao kama Husseiniya katika wilaya ya Al Kawthar mjini Saihat karibu na eneo la Qatif mashariki mwa Saudia. Taarifa hiyo imesema kitendo hicho cha kigaidi kilichopelekea watu wasio na hatua kuuawa ni ishara ya wazi ya namna magaidi wa kundi la Daesh au ISIS walivopoteza mwelekeo. ISESCO  imesistiza kuwa waliotekeleza hujuma hiyo ni 'mufsidina fil ardh' yaani watu wanaoeneza ufisadi duniani kwani hawazingatii hata chembe heshima ya maeneo ya ibada, misikiti na damu ya Waislamu.
Ikumbukwe kuwa siku ya Ijumaa Waislamu watano wa madhehebu ya Shia wameuawa nchini Saudi Arabia kufuatia hujuma ya kundi la kigaidi la Daesh au ISIS katika majlisi ya maombolezo ya siku 10 za Muharram.
Kilele cha maombolezo hayo ni siku ya 10 ijulikanayo kama Ashura wakati Waislamu hukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Mtume Muhammad , SAW, Imam Hussein AS huko Karbala.../mh

3388338

captcha