IQNA

Kituo cha Kiislamu Australia chahujumiwa, Qur’ani zavunjiwa heshima

14:06 - February 16, 2016
Habari ID: 3470142
Genge la wenye chuku dhidi ya Uislamu wamehujumu kituo cha Kiislamu Australia na kuvunjia heshima nakala za Qur’ani zilizokuwemo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kituo hicho cha Kiislamu cha Preston, Melbourne kimeharibiwa kikamilifu huku kuta zake zikiandikwa maandishi machafu. Aidha dirisha na milango yote ya kituo hicho imeharibiwa kikamilifu na inakadiriwa hasara iliyopatikana ni ya takribani dola $200,000. Kituo hicho husambaza vitabu vya Kiislamu katika eneo hilo mbali na kuandaa semina kwa ajili ya vijana Waislamu.

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na hujuma hiyo.

Polisi wamesema wanachunguza hujuma hiyo.

Wimbi la chuki dhidi ya Uislamu linashuhudiwa katika nchi za Magharibi na kuyafanya kuwaa machungu maisha ya mamilioni ya Waislamu katika nchi hizo. Nchi za Magharibi zinadai kuwa huru na kulinda haki za watu wote lakini zimeshindwa kuchukua hatua zozote za kuwalinda Waislamu.

3459077

captcha