IQNA

Bustani ya Qur'ani kujengwa katika mji mji wa Mashhad, Iran

11:48 - February 20, 2016
Habari ID: 3470151
Iran inapanga kujenga Bustani ya Qur'ani katika mji mtakatifu wa Mashhad ifikapo mwaka 2017.

Hayo yamedokezwa na Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu Iran Ali Jannati siku ya Alhamisi katika kikao cha baraza la utungaji sera kuhusu Mji Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Mji wa Mashhad umeteuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiislamu ISESCO kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2017.

Jannati amesema serikali ya Iran inatenga bajeti maalumu kwa ajili ya mradi huo wa Mashhad ili kuwezesha uwekezaji katika sekta binafsi kupitia misaada ya banki.

Kwa mujibu wa Jannati, kutajwa Mashhad kuwa mji mkuu wa kiutamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu ni fursa ya kuarifisha utamaduni na mila za Iran na kustawisha maingiliano baina ya nchi za Waislamu.

Kila mwaka ISESCO huteua miji mitatu ya Kiislamu ya nchi za Kiarabu, Afrika na Asia kuwa miji mikuu ya utamaduni ya ulimwengu wa Kiislamu kila mwaka.

3476682


captcha