IQNA

Qarii wa Iran apata zawadi ya kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Malaysia

15:26 - May 21, 2017
Habari ID: 3470989
KUALA LUMPUR (IQNA)-Mashindano ya 59 ya Kimataifa ya Qur'ani yamemalizika Jumamosi katika sherehe iliyofanyika mjini Kuala Lumpur

Washiriki wa kategoria mbali mbali walitunukiwa zawadi katika sherehe za kufunga zilizohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu akiwemo Mfalme wa Malaysia.

Jopo la majaji lilimtangaza Ustadh Hamid Alizadeh wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa mshindi katika kitengo cha qiraa baada ya kupata pointi 89.96 katika jumla ya pointi 100.

Nafasi ya pili katika kitengo hicho imechukuliwa na Hussein Tahir Shakir wa Iraq huku mwakilishi wa Malaysia Wan Fakh al Razi bin Wan Muhammad akishika nafasi ya tatu.

Nafasi za nne na tano zilischukuliwa na wawakilishi wa Canada na Singapore kwa taratibu.

Kaitka kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kikamilifu , hufadh wa Senegal, Malaysia, na Qatar walishika nafasi za kwanzi hadi tatu kwa taratibu.

Katika mashindano maalumu ya wanawake ya kuhifadhi Qur'ani zawadi tatu za kwanza zilichukuiwa na washiriki wa Nigeria, Palestina na Senegal kwa taratibu.

Kwa ujumla kulikuwa na washiriki 91 katika vitengo vya kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kutoka nchi 49 katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani ya siku sita. Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu ilikuwa ni "Udugu wa Kiisalmu kwa Msingi wa Umoja wa Umma wa Kiislamu."

Mashindano ya Kimatiafa ya Qur'ani Malaysia huandaliwa na serikali ya nchi hiyo kwa lengo la kustawisha utamaduni wa Qur'ani na kuimarisha mafundisho ya kitabu hicho kitukufu.

3599530


Hamid Alizadeh


Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha