IQNA

Waislamu nchini Uingereza; Jamii Anuai+PICHA

7:51 - May 30, 2017
Habari ID: 3471001
TEHRAN (IQNA)-Uingereza ni makaazi ya jamii anui ya Waislamu kutoka karibu pembe zote za dunia.

Historia ya Waislamu Uingereza inarejea karibu miaka 1000 iliyopita. Kwa mfano katika karne ya nane miladia, Mfalme Offa alitegeneza sarafu zilizokuwa na maandishi ya Kiislamu na Kiarabu. Sarafu hizo zilikuwa zimeandikwa "Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu".

Jamii kubwa ya Waislamu Uingereza ni kutoka eneo la Asia Kusini. Aidha kuna Waislamu wengie kutoka nchi za Kiarabu, Kiafrika na pia Waislamu kutoka wa Kusini Mashariki mwa Asia, eneo la Balkan barani Ulaya na Uturuki. Halikadhalika kuna wenyeji wengi wa Uingereza ambao wamesilimu. Kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya watu Uingereza, kuna Waislamu milioni 2.8 nchini humo kati ya watu milioni 64 nchini humo. Waislamu wameenea katika maeneo yote ya Uingereza na wamewakilishwa katika sekta zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Waislamu wanamiliki migahawa, na biasahra nyinginezo na pia wanafanya kazi katika sekta za sheria, tiba, teknolojia, usafiri, elimu, vyombo vya habari, sanaa, mitindo n.k. Aidha Waislamu ni kati ya wanamichezo na wanariadha bora Uingereza.

Waislamu wametoa mchango mkubwa katika kuifanya Uingereza iwe nchi yenye watu wa makabila na dini mbali mbali. Karibu asilimia 47 ya Waislamu Uingereza wamemzaliwa nchini humo. Kuna Waislamu 290,000 walio na umri wa kati ya miaka 9-14 huku asilimia 53 ya Waislamu wakiwa chini ya umri wa miaka 19.

Waislamu wa kwanza kuwasili Uingereza kama kundi walifika nchini humo karne ya 18 kama mabaharia maarufu kama lascars kutoka Bara Hindi. Kati ya Waingereza maarufu waliosilimu ni William Quilliam ambaye alibadilisha jina lake kuwa Abdullah Quilliam. Alizaliwa Aprili 1856 na kufarikia dunia 1932 na alikuwa wakili na malenga ambaye alianzisha msikiti wa kwanza Uingereza ambao ulijulikana kama Kituo cha Waislamu cha Liverpool. Aidha Mohammad Marmaduke Pickthall alikuwa Muingereza mwandishi wa riwaya aliyezaliwa Mkristo na kusilimu kisha akafanikiwa kuifasiri Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiingereza.

Waislamu wamejitolea sana kwa ajili ya Uingereza ambapo wengi walipigana kwa niaba ya nchi hiyo katika Vita Vikuu vya Kwanza na Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Mwaka 2016 jiji la London lilimchagua Meya wa kwanza Muislamu, Sadiq Khan, aliyekuwa wakati mmoja Waziri katika chama cha upinzani cha Laba

Leo Waislamu wanaoishi Uingereza wanatoka mataifa mbali mbali duniani huku kukiwa na idadi kubwa ya Waingereza waliosilimu. Pamoja na mchango wao mkubwa na wa kihistoria, Waislamu Uingereza wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa kubaguliwa na kutengwa na watu wenye misimamo mikali ya utaifa na chuki dhidi ya Uislamu.

Waislamu nchini Uingereza; Jamii Anuai+PICHA

Waislamu nchini Uingereza; Jamii Anuai+PICHAWaislamu nchini Uingereza; Jamii Anuai+PICHA


Waislamu nchini Uingereza; Jamii Anuai+PICHA


Waislamu nchini Uingereza; Jamii Anuai+PICHA

3604327

captcha