IQNA

Msikiti mjini Liverpool wapokea tuzo ya kuhudumia jamii

15:26 - February 25, 2022
Habari ID: 3474972
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Al-Rahma huko Liverpool nchini Uingereza umeshinda tuzo ya heshima kwa kazi yake kubwa ya uhamasishaji katika jamii mwaka jana.

Msikiti huo unaosimamiwa na Jumuiya ya Waislamu wa Liverpool, umepewa tuzo ya ‘Huduma Bora ya Uhamasishaji’ katika Tuzo ya Beacon ya Msikiti Uingereza. Kategoria ya tuzo ya 'Huduma Bora ya Ufikiaji' inatambua programu zinazotengenezwa na uongozi wa misikiti au timu kwa lengo la kufikia jamii..

Tuzo hizo ziliundwa ili kuangazia jukumu la misikiti na vituo vya Kiislamu katika jamii zao.

Mpango huo unahimiza taasisi kujitahidi kwa ubora katika njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwafikia vijana, usimamizi, uongozi, na utunzaji misikiti. Inazingatiwa jinsi wakuu wa msikiti wanavyofikia jamii isiyotumia msikitia, kama vile kualika jamii ya wasiokuwa Waislamu msikitini kwa programu au shughuli.

Msikiti wa Al-Rahma ulitunukiwa tuzo kwa kazi yake ya kupambana na kuenea kwa virusi vya Covid-19 katika jamii na juhudi ambazo imefanya kudumisha mawasiliano na jamii na kutoa msaada na uongozi muhimu wakati wa janga hilo.

Pia walifanya kazi muhimu katika kliniki ya chanjo msikitini wakati wa janga hilo na walifungua milango yao kwa jamii zote na walikuwa wakiendesha ujumbe wa chanjo pia.

Akizungumza na The Muslim News,  Dk Badr Abdullah, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu Liverpool, alisema kuutambua msikiti "kumenijaza na shukrani kubwa".

"Utambuzi huu wa bidii ya ajabu na juhudi zinazofanywa na Msikiti wa Al-Rahma kupambana na Covid-19 unathaminiwa sana," aliongeza.

Kando na sala za kila siku, msikiti huo pia umeandaa madarasa ya watoto, hafla za michezo, vikundi vya akina mama na watoto wachanga, makusanyo ya fedha kwa misaada ya Uingereza na misaada, na shughuli zingine.

Zaidi ya hayo, msikiti huo unakaribisha shule na mashirika kwa ajili ya ufahamu wa kielimu shughuli zake za kila siku. Shule moja ilisema: “Asante kwa ukaribisho mchangamfu tuliopokea na muongozaji wetu mzuri, lakini pia kila mtu Msikitini.

"Wanafunzi wetu walifanywa kujisikia wamekaribishwa na kustareheshwa katika mazingira yasiyofahamika, ambayo ni nadra sana, na yanathaminiwa sana. Wanafunzi wakiwa wanarejea shuleni walikuwa wakizungumza kuhusu jinsi walivyofurahia ugeni huo. Ukarimu na uvumilivu wenu kwa wanafunzi wetu ulifanya tukio hilo kuwa la kufurahisha zaidi na kuwaruhusu kujifunza zaidi kuhusu tamaduni na imani zingine katika mazingira tulivu”. 

3477952

captcha