Datuk Rosyam Noor amesema atatumia harakati hiyo, ambayo katika mitandao ya kijamii inajulikana kama World #QuranHour, kwa lengo la kuleta umoja katika jamii zote nchini humo.
Amesema kuna fikra potovu kuhusu Uislamu ambapo baadhi wanadhani kuwa Waislamu ni watu wapendao vita na ghasia. ‘Harakati hii inalenga kuondoa fikra mbaya kuhusu Uislamu. Tunataka watu wafahamu kuwa dini haiwezi kunasibishwa na tabia za watu wachache.”
Amesema wasiokuwa Waislamu wanakaribishwa katika harakati hiyo ya ili washuhudie mvuto uliopo katika mafundishi ya Qur’ani Tukufu.
Aidha amesema harakati haiyo ya World #QuranHour itafanyika
Agosti 31, kwa minasaba miwili. Awali siku hiyo inatazamiwa kuwa Mahujaji
katika Ibada ya Hija watakuwa wakitekeleza amani ya Wukufu huko Arafah na pili
Agosti 31 pia ni Siku ya Kitaifa ya
Malaysia.
Shughuli hiyo ya World #QuranHour itafanyika katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu Malaysia katika Msikiti wa Sultan Haji Ahmad Shah kuanzia saa tano asubuhi hadi saa saba mchana kwa wakati wa nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia.