IQNA

14:55 - June 28, 2019
News ID: 3472020
TEHRAN (IQNA)- Maisan Yahya Muhammad, ni binti wa miaka sita ambaye kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambaye amehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Binti huyo ambaye anatazamia kuanza darasa la kwanza mwakani ndiye mtoto mwenye umri wa chini zaidi aliyeweza kuhifadhi Qur'ani kikamilifu nchini UAE.
Mama yake anasema, Maisan alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu akiwa na umri wa miaka mitatu katika madrassah ya Qur'ani eneo la Sharjah.
Anaogeza kuwa, bintiye akiwa na umri wa miaka mitatu aliwahi kushiriki katika Mashindano ya Qur'ani ya Sheikh Zayed na akashifa nafasi ya saba. Wakati huo alikuwa amehifadhi Juzuu mbili.

3822455

Name:
Email:
* Comment: