IQNA

20:39 - January 15, 2020
News ID: 3472375
TEHRAN (IQNA) – Waumini wanarejea katika misikiti mitano ya kihistoira ambayo imekarabatiwa na kuanza kutumiwa baada ya hadi miongo sita.

Ukarabati wa misikiti hiyo umekamilika katika maeneo ya Makkah na Al Baha ikiwa ni sehemu ya mpango maalumu wa kukarabati misikiti ya kale.

Kwa mujibu wa mpango huo misikiti 130 itakarabatiwa kote Saudi Arabia na kazi hiyo itafanywa na mashirika ya nchi hiyo yenye utaalamu wa kukarabati turathi za utamaduni.

Misikiti ya Jarir Al-Bajali na Suleiman huko Taif, pamoja na misikiti ya Al-Malad, Al-Atawilah, na Al-Dhafir huko Al-Baha, ni misikiti iliyo karabatiwa hivi karibuni baada ya kufungwa kwa baina ya miaka  40 hadi 60.

Inadokezwa kuwa msikiti wa Jarir Al-Bajali ulijengwa wakati wa zama za mmoja kati ya masahaba wa Mtume Muhammad SAW aliyejulikana kwa jina la Jarir bin Abdullah Al-Bajali. Msikiti huo ni kati ya maeneo ya kale zaidi ya ibada katika eneo la Makkah.

3871802

 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: