IQNA

Rais Pezeshkian: Njia ya Imam (MA) ni kushirikiana na wananchi

15:25 - January 31, 2026
Habari ID: 3481873
IQNA-Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa njia ya Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ni kushirikiana na wananchi na kuwa pamoja nao.

Akihutubia katika hafla  kuhuisha ahadi ya Serikali ya Kitaifa kwa malengo ya Imam Kheomioni, katika haram ya mtukufu huyo kusini mwa Tehran, amesema kwamba nguvu na nguzo dhidi ya maadui ni wananchi wenyewe, na kwamba Serikali inapaswa kuwa mtumishi wa kweli kwa watu wake.

Kwingineko katika hotuba yake, Rais Pezeshkian amesema kuwa katika ghasia za hivi karibuni nchini zilizochochewa na tawala za kigeni, Rais wa Marekani Donald Trump, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, na watawala wa Ulaya walijaribu kuchochea vurugu na kuibua mgawanyiko ndani ya Iran.

Rais Pezeshkian amesema kuwa wahusika hao walijaribu taharuki huku wakiunga mkono makundi fulani ambapo baadhi ya watu wasio na hatia walishawishiwa katika hali hiyo na kujikuta wakiwa katika maandamano ya ghasia

Kwa mujibu wa Pezeshkian, lengo lilikuwa kuligawa taifa, kuchochea migogoro na chuki miongoni mwa wananchi, na kuibua mpasuko mkubwa ndani ya jamii.

Waandamanaji wenye silaha na magaidi wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni waliteka nyara maandamano ya amani na ya hapa na pale yaliyohusu malalamiko ya kiuchumi mnamo Januari 8 na 9.

Trump ahamasisha waziwazi matumizi ya vurugu kwa kuwataka waandamanaji wenye silaha kuchukua taasisi za serikali na kutishia kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran iwapo magaidi hao wangedhuriwa.

Vurugu hizo ambazo zilichochewa waziwazi na Marekani na utawala wa Israel, zilisababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma na binafsi, zikiwemo uharibifu mpana wa maduka, taasisi za serikali, miundombinu ya huduma za umma, pamoja na vifo vya maelfu ya raia na maafisa wa usalama.

Habari inayohusiana:

Rais wa Iran amebainisha kuwa katika maandamano ya kijamii ya kawaida, watu hawachukui silaha, hawaui wanajeshi, wala kuwasha moto magari ya wagonjwa au masoko. Alisisitiza kuwa serikali ina wajibu wa kusikiliza sauti na malalamiko ya waandamanaji na kushughulikia matatizo yao, akieleza kuwa mamlaka ziko tayari kufanya hivyo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ilikuwa wazi hali hiyo ilizidi maandamano ya kijamii ya kawaida, kwani maadui walitumia changamoto zilizokuwepo kuchochea machafuko na kuendeleza juhudi za kuligawa taifa. Pezeshkian amesisitiza kuwa uwepo wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, pamoja na mwongozo wake, umeendelea kuvuruga mipango kama hiyo mara kwa mara na utaendelea kufanya hivyo siku zijazo.

4331261

captcha