IQNA

Ayatullah Khamenei azuru Haram ya Imam Khomeini (MA), Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu

15:08 - January 31, 2026
Habari ID: 3481872
IQNA-Sherehe za kuadhimisha mwaka wa arobaini na saba tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu zimeanza kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuzuru haram haram tukufu ya Imam Khomeini (MA), muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa tovuti ya khamenei.ir, katika  kumbukumbu ya mwaka wa 47 wa ushindi wa Mapinduzi na mwanzo wa sherehe za 'Afajiri 10', Kiongozi wa Mapinduzi leo asubuhi alifika katika kaburi la Imam Khomeini (rehema za Mungu ziwe juu yake) na kusoma Fatiha kama ishara ya kuheshimu na kuenzi hadhi ya mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Ayatullah Khamenei, baada ya kusoma Fatiha na kuswali katika haram ya Imam Khomeini (MA), alimuomba Allah SWT aipe daraja za juu  roho ya Imam huyo mkubwa na mpiganaji wa njia ya haki, pamoja na mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kila mwaka, Wairani na wapenda haki kote duniani huadhimisha kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuanzia tarehe 1 hadi 11 Februari, ambazo hujulikana kama sherehe za Alfajiri Kumi. 

Habari inayohusiana:

Taifa la Iran liliuangusha utawala wa Pahlavi ulioungwa mkono na Marekani miaka 47 iliyopita, na hivyo kumaliza zaidi ya miaka 2,500 ya utawala wa kifalme nchini humo.

Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na marehemu Imam Khomeini yaliweka mfumo mpya wa kisiasa uliotegemea misingi ya Kiislamu kwa kujumuisha wananchi waliowengi.

3496248

Habari zinazohusiana
captcha