IQNA

11:29 - February 05, 2020
News ID: 3472441
TEHRAN (IQNA) –Mwanazuoni wa ngazi za juu nchini Sudan amelaani vikali mkutano wa hivi karibuni wa wa Mkuu wa Baraza la Utawala la Sudan Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa, Sheikh Abdul Hay Yusuf, mkuu wa Kitivo cha Masomo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika amesema hatua ya al Burhan kukutana na Netanyahu ni uhaini.

Amesema serikali ya sasa ya Sudan imetokana na mapinduzi ya kijeshi na hivyo haina nguvu za wananchi ili kuiwezesha kukutana na Netanyahu.

Mkutano huo ulifnayika Jumatatu katika Ikulu ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni mjini Entebbe.

Chama cha Wananchi cha Congress nchini Sudan nacho pia kimelaani vikali mkutano na kusema mkutano huo umeiaibisha Sudan.

Chama hicho cha upinzani kimetoa taarifa Jumanne usiku na kusema: "Mkutano wa Al Burhan na Netanyahu nchini Uganda unaenda kinyume na msimamo wa watu wa Sudan wa kuunga mkono Wapalestina katika mapambano yao na utawala ghasibu wa Israel."

Aidha taarifa hiyo ya Chama cha Congress imesema mkutano huo utachafua sura ya Sudan pamoja na msimamo wa kiheshima Wasudan katika kutetea watu wa Palestina. Taarifa hiyo imetaka Baraza la Utawala la Sudan litangaza rasmi kumpinga al Burhan kutokana na hatua yake hiyo.

Jana Jumanne wananchi wa Sudan waliokuwa na hasira waliandamana mbele ya ofisi ya waziri mkuu mjini Khartoum kupinga mkutano huo wa Al Burhan na Netanyahu.

Katika miezi ya hivi karibuni, utawala dhalimu wa Israel umekuwa ukitekeleza mkakati maalumu wa kuimarisha uhusiano wake na nchi za Kiafrika. Katika mkakati huo, hivi karibuni utawala huo ulitangaza kutenga kutenga bajeti ya dola milioni 700 ili kusaidia mashirika ya Kizayuni yaweze kujipenyeza katika bara la Afrika

Nchi za bara la Afrika zina utajiri mkubwa wa mafuta ya petroli, madini hasa almasi, dhahabu na urani na nukta hiyo imepelekea utawala wa Kizayuni uweke mpango maalumu wa kupora zaidi utajiri wa nchi za Afrika.

3876430

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: