IQNA

Wataalamu Wairani katika Wizara ya Ulinzi waunda kifaa cha kupima kirusi cha Corona

6:54 - February 24, 2020
Habari ID: 3472500
TEHRAN (IQNA)- Wataalamu Wairani wamefanikiwa kuunda kifaa maalumu (test kit( cha kupima kirusi cha Corona. Kifaa hicho ni cha kwanza cha aina hiyo kuundwa nchini Iran.

Shirika la Habari la Fars News limeandika  kuwa kifaa hicho cha kupima kirusi cha Corona kimeundwa na wataalamu Wairani katika Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kifaa hicho kilichoundwa nchini Iran kina uwezo wa kubaini iwapo mwanadamu ana kirusi cha  Corona mwilini na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kukabiliana na kirusi cha Corona ambacho pia kinajulikana kama COVID-19.

Tangu kuthibitishwa kwa visa vya kwanza Desemba 2019, homa ya COVID -19 ya kirusi cha Corona ilisambaa na kuwa dharura kuu ya kiafya duniani, na kuua mamia ya watu na kuambukiza maelefu ya wengine.

Homa hiyo iliripotiwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan mkoani Huabei mashariki mwa China na sasa mbali na kuenea katika mikoa 30 nchini China homa hiyo ya Corona imeenea katika zaidi ya nchi 30 zikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Australia, Italia, Thailand, Korea Kusini, Japan, Canada, Ufaransa, Umoja wa Falme za Kiarabu na Imarati.

Kwa mujibu wa takwimu, hadi sasa watu wasipungua 79,000 wameambukizwa kirusi cha Corona duniani, aghalabu wakiwa nchini China na miongoni mwao 18,000 wamepata nafuu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini huku wengine 2, 400 wakipoteza maisha.

Dalili za Corona

Dalili zake zinaonekana katika kukohoa, kupumua kwa taabu na kupata homa. Vijidudu hivyo pia vinaweza kusababisha maradhi ya kichomi yaani uvimbe kwenye mapafu unaosababisha usaha.

Kuepuka maambukizi

Jambo la kwanza ni kuzingatia ni usafi wakati wote. Pili inapasa kuepuka kukaribiana na watu wenye mafua na vikohozi vikali na pia inashauriwa kuepueka wanyama pori waliohai au waliokufa. Mtu anapaswa kunawa mikono kila mara na hasa baada ya kukaribiana na mtu mwenye maambukizi. Hata hivyo wataalamu hawatarajii kuenea kwa maambukizi ya Corona duniani kote.

3880951

captcha