IQNA

20:20 - February 24, 2020
News ID: 3472501
TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Malaysia Mahathir Mohamad amejiuzulu wadhifa huo. Hatua hiyo ya Mahathir Mohamad inatayarisha uwanja wa kuundwa serikali mpya nchini Malaysia.

Mahathir Mohamad alikabidhi hati ya kujiuzulu kwake kwa mfalme wa Malaysia jana Jumapili.

Vilevile chama chake cha Parti Pribumi Bersatu Malaysia kimetangaza kwamba, kimejiondoa katika serikali ya mseto inayotawala Malaysia ya Alliance of Hope.

Uamuzi wa Mahathir unafuatia wiki ya malumbano ya kisiasa, baada ya kuripotiwa kwamba, chama chake kilikuwa kinapanga kuunda serikali mpya ambayo itamuweka kando mrithi wake mtarajiwa, Anwar Ibrahim.

Mzozo wa sasa kati ya wapinzani hao wawili wa muda mrefu yaani Mahathir, 94, na Anwar, 72, ni wa hivi karibuni zaidi katika mivutano ya muda mrefu ya kisiasa kati ya wanasiasa hao mashuhuri nchini Malaysia. 

3881152

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: