IQNA

22:25 - August 01, 2020
News ID: 3473021
TEHRAN (IQNA) – Misikiti katika mji mkuu wa China, Beijing iliandaa Swala ya Idul Adha siku ya Ijumaa.

Misikiti hiyo ilifunguliwa Alhamisi baada ya kufungwa kutokana na hofu ya kuenea ugonjwa wa COVID-19.

Hatahivyo Waislamu hawakuweza kuchinja kutokana na tahadahri za kuzuia kuenea COVID-19.

Waislamu walioshiriki katika Swala ya Idi walizingatia kanuni za kiafya za kutokaribiana huku vipimo vya kiwango cha joto mwilini vikichukuliwa kabla ya kuingia msikitini.

Jumuiya ya Kiislamu ya China imetoa taarofa ikiwapongeza Waislamu kwa mnasaba wa siku kuu ya Idul Aadha na ushirikiano katika vita dhidi ya COVID-19.

Sherehe za Idi kote duniani zilikuwa tafautia na miaka iliyopita kutokana na ivingiti vilivyowekwa na nchi mbali mbali kuzuia kuenea COVID-19.

3913786

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: