IQNA

Idul Adha na Idul Fitr kuwa sikuu rasmi katika jimbo la Washington, Marekani

19:16 - April 11, 2025
Habari ID: 3480522
IQNA- Sheria mpya imetangaza Idul Adha na Idul Fitr kuwa sikukuu rasmi katika jimbo la Washington nchini Marekani.

 Muswada wa Nambari 5106 wa Bunge la Seneti, uliopitishwa na Gavana Bob Ferguson katika Kituo cha Kiislamu cha Tacoma, unafanya Washington kuwa jimbo la kwanza nchini Marekani kutambua rasmi Idi au sikukuu hizi mbili za Kiislamu.

Zaidi ya Waislamu 100,000 wanaadhimisha sikukuu hizi katika jimbo hilo. Seneta Yasmin Trudeau, mpendekezaji wa muswada huo, alisema kuwa kuwepo kwa jamii ya Waislamu wakati wa kutiwa saini kulionyesha umuhimu wake.

Mwakilishi Osman Salahuddin alisema kuwa wanafunzi Waislamu mara nyingi hukosa hafla muhimu za Idi kutokana na kutokuwepo katika sheria.

Sasa sheria hii inaruhusu wafanyakazi kuchukua likizo mbili zisizolipwa kila mwaka kwa sababu ya kusherehekea sikukuu hizi mbili. Pia, taasisi za elimu ya juu zitalazimika kupangilia tena mitihani au shughuli za shule kwa sababu ya wanafunzi Waislamu wanaosherehekea sikuukuu hizi.

Idul Fitr huadhimishwa mwisho wa Ramadhani, mwezi wa kufunga na ibada. Idul Adha nayo huadhimishwa wakati wa kukamilika ibada ya Hija. Sikukuu hizi huambatana na mikusanyiko ya kifamilia na kijamii.

 

3492644

captcha