IQNA

TEHRAN (IQNA) - Mijumuiko ya Jioni ya Ashura imefanyika katika miji mbali mbali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Siku hii ya Jioni ya Ashura katika utamaduni na fasihi ya Iran hujulikana kama Sham-e Ghariban. Jioni ya Ashura na baada ya kuchomwa moto mahema ya wafuasi na familia ya Imam Hussein AS ambaye ni mjukuu mpendwa wa Mtume Mtukufu SAW,  watoto mayatima waliachwa wakihangaika jangwani huku waovu na makatili waliotekeleza mauaji hayo ya kutisha dhidi ya kizazi cha Mtume wakianza kusherehekea ushindi wao wa kidhahiri. Askari wa maadui walikuwa wakicheka kwa sauti za juu huku wakicheza densi. Baada ya kusherehekea kwa muda mrefu na kuchoka hatimaye waliingia kwenye mahema yao na kulala, huku wanawake wachache waliobakia na watoto wa kizazi cha Mtume wakilala nje kwenye baridi kali baada ya mahema yao kuteketezwa moto na maadui. 

 

 

 

 
Kishikizo: ashura ، imam hussein as