IQNA

Maombolezo Makubwa Yafanyika Usiku wa Ashura huko Karbala

18:09 - July 06, 2025
Habari ID: 3480904
IQNA-Maelfu kwa maelfu ya waombolezaji walikusanyika katika mji mtukufu wa Karbala nchini Iraq, usiku wa Ashura, kuadhimisha kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS), katika mojawapo ya hafla kubwa zaidi za kidini katika kalenda ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Iraq, halaiki kubwa ya waombolezaji kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq na nchi nyingi duniani walishiriki katika maombolezo hayo yaliyofanyika kwenye Haram ya Imam Hussein (AS) na ndugu yake wa kambo Abbas ibn Ali (AS), huko Karbala Jumamosi usiku.

Hafla hiyo iliadhimisha usiku wa Ashura, yaani tarehe 10 ya mwezi wa Muharram wa Kiislamu, siku ambayo huadhimisha kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), pamoja na maswahaba wake waliouawa katika vita vya Karbala mnamo mwaka 61 Hijria.

Mjumuiko huo ulijumuisha nyimbo za maombolezo za jadi na dua maalumu, ambapo washirki waliwakumbuka mashahidi wa uwanda wa Karbala.

Shirika hilo la habari liliripoti kwamba “idadi kubwa ya waombolezaji na wapenzi wa Imam Hussein (AS) walifua mishumaa kwa kumbukumbu ya mashahidi wa ardhi ya Nainawa”—jina la kihistoria la eneo la Karbala.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq ilitangaza Jumapili kuwa zaidi ya wafanyaziara milioni 1.176 wameingia nchini humotangu kuanza kwa mwezi wa Muharram. Katika mkutano na waandishi wa habari, Kanali Abbas al-Bahadli, msemaji wa wizara hiyo alisema kuwa jumla ya mawkib 833 zimesajiliwa rasmi katika mji wa Karbala kwa ajili ya maadhimisho ya Ashura, ikiwa ni pamoja na moukeb 10 kutoka nje ya Iraq. Kituo hivyo hutoa huduma kama vile chakula, maji, na malazi kwa mahujaji.Mawkib ni vituo vya huduma vilivyo katika maeneo ya kidini ya Waislamu wa madhehebu ya Shia au wakati wa matukio ya kidini ya Mashia ambapo wafanyaziara na watu wanaweza kupokea chakula, chai, na sharbat (vinywaji vitamu) na kupata sehemu ya kupumzika.

 

.

 

Aidha, alieleza kuwa Idara ya Ulinzi wa Raia ya Iraq imeweka vikosi katika mitaa ya kale ya Karbala kwa ajili ya kukabiliana haraka na dharura kama vile moto au ajali nyingine.

Ziyara ya Ashura ni mojawapo ya hafla muhimu zaidi kila mwaka kwa Waislamu wa madhehebu ya Shia duniani kote, ikivuta mamilioni ya wageni kila mwaka kuelekea kwenye kaburi la Imam Hussein (AS), ambaye anaheshimiwa kama alama ya kupinga dhulma na kusimamia haki.

/3493727

Kishikizo: ashura imam hussein as
captcha