IQNA

Mjumbe wa UN: Karbala ina nafasi maalum mioyoni mwa wote

19:06 - July 06, 2025
Habari ID: 3480907
IQNA – Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq una nafasi ya kipekee katika mioyo ya watu wote.

Katika taarifa rasmi, Gavana wa Karbala, Nasayf Jassim Al-Khattabi, alimpokea Mohamed Al-Hassan, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Iraq, siku ya Jumamosi.

Maafisa hao walijadili uwezekano wa ushirikiano kati ya mkoa wa Karbala na mashirika ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Gavana Al-Khattabi alisifu juhudi za kibinadamu zinazofanywa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq na akaonesha nia ya Karbala kushirikiana na taasisi za kimataifa ili kuinua hadhi ya mkoa na kuwahudumia wananchi wake.

Katika mkutano huo, Gavana alieleza kwa kifupi nafasi ya Karbala katika historia ya kidini na kisiasa, na mchango wake mkubwa kama kituo cha  milioni wafanyaziara kila mwaka. Pia alibainisha juhudi za mkoa kuboresha miundombinu, huduma za kijamii, na sekta nyingine muhimu.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, ambaye alitembelea maeneo mbalimbali ya Karbala, alieleza mji huo kama “mji mkuu wa kiroho wenye nafasi maalum katika mioyo ya kila mtu.”

Alisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia juhudi za maendeleo na ujenzi upya wa Karbala, hasa ikizingatiwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa ngazi nyingi. Alisema kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu maendeleo chanya yanayoendelea katika mji huo.

Wakati wa siku za kuelekea Ashura siku ya kumi ya mwezi wa Muharram kwa kalenda ya Hijria, inayoadhimisha kifo cha kishahidi cha Imam Hussein (AS) Karbala imepokea mamilioni ya wafanyaziara wanaofika kushiriki maombolezo ya Muharram.

/3493720

captcha